1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

UN: Israel inawatesa wafungwa wa Kipalestina

31 Julai 2024

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imetoa ripoti inayosema wafungwa wa Kipalestina wanaozuiliwa na mamlaka ya Israel tangu mashambulizi ya Oktoba 7 wanakabiliwa na mateso makubwa.

https://p.dw.com/p/4ix56
Wafungwa wa Palestina
Ripoti ya Umoja wa Mataifa yasema Israel inawatesa wafungwa wa Kipalestina Picha: Bashar Taleb/AFP

Mateso hayo yanajumuisha kumwagiwa maji wakiwa wamefungwa kitambaa kilichouziba uso na pua, kunyimwa nafasi ya kulala vya kutosha, kuchomwa kwa umeme pamoja na unyanyasaji wa aina nyingine.

Ripoti hiyo inasema huduma ya magereza ya Israeli ilikuwa imewashikilia zaidi ya
wafungwa hao 9,400 kufikia mwisho wa Juni, na kwamba wengine wameshikiliwa kisiri na kunyimwa huduma za mawakili ama heshima kwa haki zao za kisheria.

Israel yashambulia shule huko Gaza na kuuawa watu 30

Muhtasari wa ripoti hiyo, kulingana na mahojiano na wafungwa wa zamani na vyanzo vingine, imeshutumu idadi kubwa ya wafungwa wakiwemo wanaume, wanawake, watoto, waandishi wa habari na watetezi wa haki za binadamu
na kusema vitendo kama hivyo vinaleta wasiwasi kuhusu hali ya kuzuiwa kwa watu kiholela.

Katika taarifa, mkuu wa haki za kibinadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Türk, amesema ushahidi huo uliokusanywa na ofisi yake na mashirika mengine, unaashiria vitendo vingi vya kutisha vinavyokiuka wazi sheria ya kimataifa ya haki za binadamu.