1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Walinzi wa mpakani wa Uturuki watuhumiwa kuwatesa Wasyria

27 Aprili 2023

Ripoti ya shirika la kimataifa la kutetea haki za binaadamu imewashutumu walinzi katika mpaka wa Uturuki kwa kuwapiga risasi, kuwatesa na kutumia nguvu kupita kiasi dhidi ya raia wa Syria wanaotaka kuikimbia nchi yao

https://p.dw.com/p/4Qctt

Ripoti hiyo imeishinikiza Uturuki kuwachunguza walinzi hao wa mpakani na kuwawajibisha wote waliokiuka haki za binaadamu ikiwa ni pamoja na mauaji ya kiholela na kuongeza kuwa mauaji hayo ya kuchukiza ni sehemu ya ukatili wa walinzi hao wa mpaka wa Uturuki ambao serikali imeshindwa kuwazuia au kuwachunguza ipasavyo.

Soma pia: Mawaziri wa Ulinzi wa Urusi, Iran, Uturuki na Syria wakutana Moscow

Takriban wakimbizi milioni 3.6 waliosajiliwa kutoka Syria, wako katika mpaka kati ya taifa hilo na Uturuki, hii ikiwa ni kulingana na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR.

Vita vya nchini Syria vya tangu mwaka 2011 vimesababisha vifo vya karibu watu nusu milioni na kusababisha wengine kuyakimbia makazi yao.