1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rishi Sunak kuwa waziri mkuu mpya nchini Uingereza

Saleh Mwanamilongo
24 Oktoba 2022

Sunak anachukuwa nafasi hiyo kufuatia kipindi cha mtikisiko mkubwa wa kisiasa kushuhudiwa katika historia ya Uingereza.

https://p.dw.com/p/4IcOB
UK Premierminister Rishi Sunak
Picha: Stefan Rousseau/empics/picture alliance

Rishi Sunak anajiandaa kuwa waziri mkuu mpya nchini Uingereza baada ya mpinzani wake katika kinyang'nyiro hicho Penny Maudaunt kujiondowa. Sunak anachukuwa nafasi hiyo kufuatia kipindi cha mtikisiko mkubwa wa kisiasa kushuhudiwa katika historia ya Uingereza. Graham Brady mwenyekiti wa wabunge wa chama cha Conservative anaehusika na masuala ya uongozi alimthibitisha Sunak kuchukua nafasi hiyo.

Mwenyekiti wa chama cha Conservative Jake Berry ametoa mwito kwa chama hicho kushikamana, kumuunga mkono Rishi Sunak mwenye umri wa miaka 42 baada ya ushindi wake leo Jumatatu. Katika taarifa yake Berry amesema Sunak ana kazi muhimu ya kuzikabili changamoto zinazoikumba nchi hiyo.

Rishi Sunak amewaambia wabunge wa chama cha Conservative kwamba lengo lake la mwanzo ni kuweka uthabiti wa kiuchumi.