Rishi Sunak, Olaf Scholz walaani jaribio la mapinduzi Niger
2 Agosti 2023Matangazo
Taarifa iliyotolewa na ofisi ya Waziri Mkuu huyo wa Uingereza imeeleza kuwa viongozi hao wawili wamejadili kuhusu hali nchini Niger baada ya jeshi kumuondoa madarakani Rais aliyechaguliwa kwa njia ya demokrasia, Mohamed Bazoum.Ufaransa na nchi kadhaa za Magharibi zimekuwa zikiwahamisha raia wake kutoka taifa hilo la Afrika Magharibi kwa kutumia ndege za kijeshi tangu wiki iliyopita.Wizara ya mambo ya nje ya Ujerumani imehimiza raia wake walioko nchini Niger kuchukua fursa ya mamlaka ya Ufaransa kwa kuabiri ndege hizo.