Robben mchezaji bora wa nusu ya kwanza ya msimu
5 Januari 2015Matangazo
Robben alitawala kura hiyo, iliyoendeshwa na jarida la michezo la Kicker na kutangazwa leo Jumatatu, akipata asilimia 46.7, akiwatangulia mchezaji wa kati wa Wolfsburg Kevin de Bruyne pamoja na mshambuliaji wa Eintracht Frankfurt Alexander Meier.
Katika uchaguzi mwingine Manuel Neuer wa Bayern Munich ametajwa kama mlinda mlango bora, Karim Bellarbi wa Leverkusen ameteuliwa kama mchezaji chipukizi bora , na Markus Weinzierl wa Augsburg amekuwa kocha bora wa mzunguko wa kwanza.
Mwandishi: Sekione Kitojo / rtre , afpe , dpae
Mhariri: Iddi Ssessanga