1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rosberg ni bingwa wa dunia

28 Novemba 2016

Nico Rosberg hatajulikana tu kuwa mwanawe bingwa wa Formula One Keke Rosberg. Dereva huyo Mjerumani sasa ni bingwa wa dunia baada ya kutwaa taji lake jana na kuyafikia mafanikio ya babake ya mwaka wa 1982

https://p.dw.com/p/2TNwh
Formel 1 Vereinigte Arabische Emirate in Abu Dhabi - Weltmeister Nico Rosberg, Deutschland
Picha: picture-alliance/dpa/V. Xhemaj

Nafasi ya pili aliyopata Rosberg katika nafasi ya pili katika mashindano ya mwisho ya msimu mkondo wa Abu Dhabi Grand Prix ilitosha kumpokonya taji mwenzake wa timu ya Mercedes Lewis Hamilton na kumzuia mpinzani wake huyo mkali kushinda taji lake la tatu mfululizo na lake la nne kwa jumla. Rosberg alimaliza msimu akiwa na pointi 385 dhidi ya Hamilton aliyekuwa na 380.

Formel 1 | Grand Prix Abu Dhabi | Weltmeister Nico Rosberg
Nico Rosberg akisherehekea ubingwa wakePicha: Getty Images/C. Mason

Alipoulizwa kama alifurahia mashindano hayo, Rosberg alijibu "Hapana. Hayakuwa mashindano yaliyonifurahisha kabisa maishani mwangu. Kulikuwa na ushindani mkali mwanzoni na pia mwishoni, na hasa katika mizunguko ya mwisho, hivyo nna furaha yamekamilika"

Muingereza Hamilton ambaye alishinda mbio hizo, alionekana kupunguza mwendo wake na hata kupuuza maagizo ya maafisa wa timu yake waliomtaka aongeze kasi. Viongozi wa Mercedes wamesema watatathmini kama watamchukulia hatua. Mjerumani Sebastian Vettel alimaliza katika nafasi ya tatu kwenye mashindano hayo ya Abu Dhabi.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/AP/DPA/reuters
Mhariri: Yusuf Saumu