1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MichezoUhispania

Rubiales akana mashitaka dhidi yake

15 Septemba 2023

Rais wa zamani wa shirikisho la soka la Uhispania Luis Rubiales amekanusha kufanya makosa yoyote alipohojiwa na jaji anayechunguza sakata la kumpiga busu mchezaji wa timu ya taifa ya Uhispania Jennifer Hermoso.

https://p.dw.com/p/4WOEg
Aliyekuwa rais wa shirikisho la soka la Uhispania Luis Rubiales akiwa anafurahia ubingwa wa Kombe la Dunia kwa wanawake pamoja na Jennifer Hermoso.
Aliyekuwa rais wa shirikisho la soka la Uhispania Luis Rubiales akiwa anafurahia ubingwa wa Kombe la Dunia kwa wanawake pamoja na Jennifer Hermoso. Picha: Noe Llamas/Sport Press Photo/ZUMA Press/picture alliance

Jaji Francisco de Jorge mapema wiki hii alimuamuru Rubiales kujibu maswali mbele ya mahakama ya kitaifa ya Uhispania juu ya sakata hilo la busu.

Ofisi ya muendesha mashtaka wa serikali imesema Rubiales amekanusha mashtaka yote yaliyokuwa yakimkabili wakati akijibu maswali mbele ya jaji katika kikao cha faragha kilichokuwa kinasikiliza kesi hiyo.

Rubiales na wakili wake Olga Tubau hawakutaka kuzungumza na waandishi wa habari nje ya mahakama.

Wiki iliyopita, waendesha mashtaka wa serikali walimshtaki Rubiales kwa unyanyasaji wa kijinsia. Kulingana na Hermoso, Rubiales alimshinikiza amtetee mara baada ya sakata hilo kuibuka.

Wakili wa Hermoso Carla Vall i Duran, amesema ameridishwa na kikao cha kusikiliza kesi hiyo.