1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ruto: Maandamano lazima yakomeshwe, upinzani wahimiza 'haki'

22 Julai 2024

Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga amesisitiza jana kuwa "haki" ndio sharti la lazima kabla ya mazungumzo yoyote na serikali baada ya mapigano makali.

https://p.dw.com/p/4iaKZ
Nairobi, Kenya | Mwandamananaji wakiwaambia jambo askari wa kutuliza ghasia.
Mmoja wa waandamanaji akiwakabili askari wa kutuliza ghasia Kenya ambao wamejihami.Picha: TONY KARUMBA/AFP/Getty Images

Odinga aliyasema hayo huku Rais William Ruto akionya kwamba machafuko yanaweza "kuharibu" nchi hiyo. Odinga mqwenye umri wa miaka 79, amesema kwamba lazima kila mwathirika wa ukatili wa polisi katika maandamano alipwe fidia kwanza na haki itendeke kabla ya mazungumzo.

Licha ya Ruto kuondoa sera ya nyongeza ya kodi, maandamano yameendela kwa wiki kadhaa kote nchini Kenya na sasa upinzani umeitisha maandamano mapya wiki ijayo.

Soma pia:Rais wa Kenya amerejea sehemu kubwa ya mawaziri wa zamani

Jana Jumapili Ruto aliahidi kuwakomesha "waporaji" na "wauaji" ambao amesema "wanahatarisha usalama wa nchi " akiongeza kwamba raia wake wanataka taifa lenye amani na utulivu, na masuala ya Kenya yatatatuliwa kwa njia za kidemokrasia.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW