Ruto ataka dunia iwekeze kwenye nishati salama Afrika
25 Septemba 2024Matangazo
Akizungumza kwenye mkutano wa kilele wa nishati jadidifu siku ya Jumanne (Septemba 24), Rais William Ruto wa Kenya alisema ulimwengu unapaswa kuwekeza kwenye nishati hizo barani Afrika kama sehemu ya ahadi waliyotowa kwenye mkutano wa kilele wa mazingira mwaka jana, COP28, ambapo mataifa makubwa yalisema yangeliongeza mara tatu zaidi uwezo wa kuwa na nishati salama kufikia mwaka 2030.
Ruto alisema, kinyume chake, bara la Afrika linapata chini ya asilimia 50 ya uwekezaji wa nishati jadidifu licha ya kuwa na asilimia 60 ya fursa za nishati hiyo ulimwenguni.
Rais huyo wa Kenya alisema Afrika ina utajiri wa nishati salama lakini halina uwezo wa kuzifikia.