Rais wa Kenya William Ruto Jumatano alitangaza awamu ya pili ya baraza lake la mawaziri ambalo limewajumuisha wanasiasa wa vyama vya upinzani. Awali rais huyo wa Kenya alipinga kuhusu serikali ya kile kinachoitwa "nusu mkate" lakini kwa sasa amewajumuisha wanasiasa hata wale walikokuwa wakimpinga na kumkejeli waziwazi. Suleman Mwiru amezungumza na Herman Manyora.