MigogoroUbelgiji
NATO: Wanajeshi wa Korea Kaskazini wamepelekwa Urusi
28 Oktoba 2024Matangazo
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO, Mark Rutte amesema anaweza kuthibitisha kwamba wanajeshi wa Korea Kaskazini wamepelekwa nchini Urusi na sehemu ya wanajeshi hao wamepelekwa katika jimbo la Kursk.
Rutte alikuwa akizungumza na waandishi habari baada ya maafisa wa NATO na wanadiplomasia kuusikiliza ujumbe wa Korea Kusini.
Amesema kuongezeka kwa ushirikiano wa kijeshi kati ya Urusi na Korea Kaskazini ni kitisho kwa usalama wa eneo zima la Indo Pasifiki pamoja na kanda ya Ulaya, mataifa ya Caucasus na Asia ya Kati.
Kadhalika kwa mujibu wa katibu mkuu huyo wa Jumuiya hiyo ya ushirikiano wa kijeshi, zaidi ya wanajeshi 600,000 wa Urusi wameuwawa au kujeruhiwa kufuatia uvamizi wake nchini Ukraine.