Rwanda: Wengine watano wafa kwa Marburg
2 Oktoba 2024Matangazo
Kwa mujibu wa wizara ya afya ya taifa hilo dogo la Afrika Mashariki, karibu watu 29 wamethibitishwa kuambukizwa ugonjwa huo tangu ulipozuka Septemba 27.
Wizara hiyo ilisema watu 19 miongoni mwao wametengwa na kuendelea kutibiwa kote nchini humo.
Soma zaidi: Sita wafa kwa Marburg Rwanda
Kituo cha Kudhibiti Magonjwa Barani Afrika (CDC) kilisema siku ya Jumanne (Oktoba 1) kwamba wengi wa wagonjwa ni wahudumu wa afya na tayari wamewafuatilia zaidi ya watu 290 waliokaribiana nao.
Virusi vya Marburg husambaa kwa kugusa majimaji ya mgonjwa.