AfyaRwanda
Rwanda yaanza kutoa chanjo ya Marburg
6 Oktoba 2024Matangazo
Akizungumza na waandishi habari mjini Kigali, waziri wa Afya Sabin Nsanzimana amesema zoezi la kuchanja waathiriwa limeanza siku ya Jumapili.
Nsanzimana ameeleza watakaopewa kipaumbele kwanza ni wale "walio hatarini zaidi, hasa wafanyikazi wa afya katika vitengo mbalimbali vya matibabu.
Kisa cha kwanza cha virusi vya Marburg nchini Rwanda kiligunduliwa mwishoni mwa Septemba, ambapo watu 46 wameambukizwa, 12 wamefariki kutokana na homa hiyo.
Dalili za Marburg ni pamoja na homa kali, maumivu makali ya kichwa, uchovu ndani ya siku saba za kuambukizwa, kichefuchefu, kutapika na kuharisha.