Baada ya Tume Huru ya Wataalamu wa Umoja wa Mataifa kuitaja Rwanda kwamba inawaunga mkono waasi wa M23 wanaokabiliana na serikali ya Kinshasa, Naibu Msemaji wa serikali ya Kigali Alain Mukurarinda, ameeleza kuwa shutma dhidi ya nchi yake hazisaidii lolote isipokuwa kudhoofisha juhudi za kikanda za kuleta hali ya usalama mashariki mwa Kongo. Sikiliza ripoti ya Sylvanus Karemera.