1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Salah miongoni mwa wawaniaji wa tuzo ya mchezaji bora Afrika

25 Novemba 2019

Mohamed Salah yuko kwenye orodha iliyotolewa jana ya majina 30 ya wanaowania tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka wa 2019 barani Afrika. Mmisri Salah anaiwinda tuzo hiyo kwa mara ya tatu

https://p.dw.com/p/3TgUz
Ghana Fußballer Mohamed Salah in Accra
Picha: Getty Images/AFP/U. Ekpei

Salah ambaye alishinda tuzo hiyo mwaka jana, ni mmoja wa nyota 10 wanaocheza katika Premier League walio kwenye orodha hiyo, ambayo inawajumuisha wenzake wa Liverpool Sadio Mane na Naby Keita.

Mbwana Samatta anayekipiga Genk ya Ubelgiji pia anawania tuzo nhiyo. Wengine ni Pierre-Emerick Aubameyang na Nicolas Pepe wa Arsenal na Jordan Ayew na Wilfired Zaha wa Crystal Palace. Wengine ni Riyad Mahrez wa Manchester City, Wilfred Ndidi (Leicester City) na Mahmoud 'Trezeguet' Hassan (Aston Villa).

Mmisri Salah analenga kubeba tuzo hiyo kwa mara ya tatu, lakini huenda akashindwa mara hii na Msenegal Mane, ambaye kwa sasa ana msimu mzuri sana katika Liverpool. Mane aliisaidia Senegal kutinga fainali ya Afcon 2019, ambapo walifungwa 1 – 0 na Algeria mjini Cairo