Sanaa au Sayansi? Macho ndio yanajua
Mwaka huu tuzo ya "Wellcome Image" imesheherekea miaka 20, kama hujawahi kuisikia, wakati ndio huu. Picha hizi inatupa fursa ya kuona dunia ya sayansi, na jicho ikiwa ndio madakuu.
Macho madogo ya nguruwe mduchu
Hapa, tunaweza kuona jicho la nguruwe mdogo - au katika matumizi ya teknolojia ya kuvuta picha ya 3D. Picha hii ni mchanganyiko wa matumizi ya CT scanning yaani chombo cha kutambaza na 3D. Sehemu ya mbali ya upande wa kulia ni kiini cha macho cha ngisi huyu. Mishipa ya damu inayosambaza damu pia inaonekana vizuri.
Ngisi mdogo mwenye mvutio
Ngisi huyu mdogo mwenye mvutio anajulikana kama "Hawaiian bobtail squid". Ana urefu wa milimita 33-35 na anatoka katika bahari ya kisiwa cha Hawaii. Usiku ngisi huyu huwinda katika maeneo ya mwamba tumbawe. Kamba ndio chakula chake kikuu. Wakati wa mchana hujificha katika mchanga. Kifuko cha uwino kinaonekana wazi katika picha hii.
Utata wa joto kubaki
Katika picha hii ya njiwa, mpambanuo unaoitwa "BriteVu" umetumika, umewezesha mishipa ya damu kuonekana. muungano huu tata ni muhimu katika kudhibiti joto la mwili la njiwa. Ndege mara nyingi husimama kwa mguu mmoja ili joto lao la mwili lisitumike haraka. Picha hii imepigwa kwa kutumia CT scanner au chombo cha kutambaza.
Ubongo juu ya kibanzi cha plastiki
Hapa wachunguzi walikuwa wakichunguza jinsi gani shina la seli za nyuroni zinavyokuwa juu ya rojo la sanisi. Baada ya wiki mbili tu, rangi nzito ya zambarau ya shina la seli imetoka nyuzi za mishipa ya kijani. Kwa kuotesha ogani au sehemu ya mmea au mwili juu ya kipenza cha plastiki, wachunguzi wanaweza kutabiri nguvu ya kuweza kutibu na nguvu ya sumu katika chanjo.
Upinde wa mvua wa Plasenta
Picha hii inaonyesha ukuwaji wa Plasenta ya panya, ambayo inaweza kusababisha kutoka kwa kudanganywa ya mfumo wa kinga ya mama. Plasenta hizo zilichunguzwa baada ya siku 12 katika kipindi cha siku 20 cha ujauzito. Wachunguzi wanataka kufahamu na kukinga matatizo wakati wa mimba. Picha hii imetengenezwa kupitia njia ya microscopy yaani hadubini.
Mwonekano wa panya
Hapa tunaona sehemu nyeti ya ndani ya jicho la panya. Mishipa ya bluu ambayo inasambaa nje kutoka katikato inaonekana wazi. Seli ya ndani kabisa inaonekana kwa rangi nyekundu. Hizi ni seli maalumu za mfumo wa mishipa inayohusika na hisia ambazo zina kazi nyingi, kwa mfano kusaidia kutengeneza ubongo au uti wa mgongo wakati wa ajali.
DNA wazi
Hapa tunaona DNA yaseli ya pafu la binadamu. Hiki ni kiini hasa cha seli. Upana wa katika picha hii ni milimita 0.084
Mtazamo wa Mboni
Picha hii inaonesha jinsi gani mboni bandia inawekwa katika jicho. Mboni ya bandia inatengenezwa kutokana na silikoni iliyounganishwa na vikamatio viwili. Mgonjwa kwenye picha hii ameweza kuona tena kwa asili mia baada ya matibabu haya
Samaki mwenye alama za kama pundamilia
Samaki huyu ni mdogo sana lakini bado maarufu katika sehemu za uchunguzi wa sayansi. Kijisamaki hiki kina nguvu, kinazaliana haraka na kina mifumo muhimu ya kifisiolojia pamoja binadamu. Hapa, genetiki imetambulisha geni inayotoa rangi nyekundu wakati wa hali maalumu. Hii ni sehemu ya kusoma tabia ya samaki kwa karibu.
Nywele za paka zilisimama
Picha hii inaonyesha ngozi ya paka, zikwemo nywele (rangi ya manjano), sharubu na pia rangi ya manjano) na Usambazaji wa damu (rangi nyeusi ). Sampuli hii ni tangu ya enzi ya Victoria. Mishipa ya damu wakati huo ilikuwa ikidungwa shindano ya rangi ili iweze kuonekana katika sehemu ya tishu, utaalamu huu ndio ulikuwa unaanza kuvumbuliwa wakati huo. Picha hii ina upana wa milimita 12.