SAO PAULO: Ban Ki Moon azuru Brazil
11 Novemba 2007Matangazo
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, amesafiri leo kwenda nchini Brazil kuhudhuria mkutano juu ya mabadiliko ya hali ya hewa.
Ziara ya Ban Ki Moon nchini Brazil inafanyika baada ya ziara nyingine aliyoifanya eneo la kaskazini la Antarctica.
Katibu mkuu huyo alifanya ziara hiyo katika eneo hilo kujionea kwa macho yake jinsi theluji inavyoyeyuka na kuanguka baharini na pia uharibu wa mazingira unaosababishwa na binadamu.
Ban Ki Moon ni katibu mkuu wa kwanza wa Umoja wa Mataifa kulitembelea eneo la Antarctica.