Saudia kuitambua Israel iwapo mzozo wa Gaza utasuluhishwa
16 Januari 2024Matangazo
Mwanamfalme Faisal bin Farhan amesema, wanakubali kuwa amani ya kikanda inajumuisha pia amani kwa Israel japo hilo linaweza kutokea kupitia kuitambua Palestina kama taifa.
Alipoulizwa wakati wa kongamano la kiuchumi la dunia linalofanyika Davos iwapo Saudi Arabia inaweza kuitambua Israel kama sehemu ya makubaliano mapana ya kisiasa, mwanamfalme huyo alijibu, "Hakika."
Waziri huyo wa mambo ya nje ya Saudi Arabia ameeleza kuwa, suala la kupatikana kwa amani ya kikanda kupitia uundwaji wa taifa la Palestina ni "jambo ambalo wamekuwa wakilifanyia kazi na utawala wa Marekani" na kwamba limekuwa muhimu zaidi wakati huu kwa kuzingatia kinachoendelea katika ukanda wa Gaza.