1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Saudi Arabia kuwa mwenyeji wa mkutano wa kimataifa wa COP16

29 Novemba 2024

Saudi Arabia wiki ijayo itakuwa mwenyeji wa mkutano wa Umoja wa Mataifa wa COP16 kuhusu uharibifu wa ardhi na kuenea kwa jangwa.

https://p.dw.com/p/4nYfQ
Mkutano uliopita wa COP16 Colombia
Mkutano uliopita wa COP16 ColombiaPicha: Camilo Rodriguez/REUTERS

Saudi Arabia wiki ijayo itakuwa mwenyeji wa mkutano wa Umoja wa Mataifa wa COP16 kuhusu uharibifu wa ardhi na kuenea kwa jangwa huku taifa hilo likijieleza kuwa mtetezi wa mazingira licha ya kukosolewa kwa jukumu lake katika mazungumzo ya wiki iliyopita ya mabadiliko ya tabianchi ya COP29 nchini Azerbaijan.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameutaja mkutano huo wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Kupambana na Kuenea kwa Jangwa (UNCCD) kuwa hatua muhimu ya lengo kuu la kulinda ardhi pamoja na kukabiliana na ukame.

Naibu waziri wa mazingira wa Saudi Arabia Osama Faqeeha, ameliambia shirika la habari la AFP kwamba nchi yao ni jangwa na inakabiliwa na hali mbaya zaidi ya uharibifu wa ardhi ambayo ni kuenea kwa jangwa.

Wanaharakati wameishtumu nchi hiyo ambayo ni msafirishaji mkubwa wa mafuta duniani, kwa kujaribu kuhujumu wito wa kukomesha matumizi ya nishati ya visukuku katika mkutano wa COP29.