Watoto 498 wamekufa kwa njaa katika vita vya Sudan
22 Agosti 2023Matangazo
Katika ripoti yake, shirika hilo limesema vifo hivyo vimetokea katika kipindi cha miezi minne ya vita, kati ya majenerali wawili hasimu. Kwa mujibu wa shirika moja linalofuatilia mizozo, takriban watu 5,000 wameuawa na wengine zaidi ya milioni 4 wamekimbia makaazi yao.
Shirika la Save the Children limelazimika kufunga vituo vyake 57 vya lishe tangu vita vilipoanza na kwamba shehena zake zinazidi kupungua katika maeneo 108 ambako bado linafanya kazi.
Mapigano yaenea Sudan huku hofu ikizidi Darfur
Katika taarifa yake ya wiki iliyopita, mkuu wa mashirika 20 ya misaada ya kimataifa, alitahadharisha kwamba zaidi ya Wasudan milioni 6 wamo kwenye ukingo wa kukabiliwa na baa la njaa.
Mapigano yameendelea hususan katika miji ya Khartoum na Darfur.