Scholz alaani shambulizi la Hamburg
10 Machi 2023Matangazo
Scholz ameliita shambulizi hilo kama ''kitendo cha ukatili.''Ameandika leo katika ukurasa wake wa Twitter kwamba yuko pamoja na wahanga na familia zao, na vikosi vya usalama ambavyo vilikabiliana na opersheni ngumu. Polisi ya Ujerumani imesema watu wanane wameuawa, akiwemo mshukiwa wa uhalifu huo.
Taarifa ya gazeti la Bild imeeleza kuwa watu waliouawa ni saba na takribani watu wengine wanane wamejeruhiwa. Aidha katika taarifa yake, Mashahidi wa Yehova wameelezea kusikitishwa na shambulizi hilo la kutisha dhidi ya wafuasi wake. Polisi inalichunguza shambulizi hilo.