1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUkraine

Scholz apinga ombi la Ukraine kujiunga na NATO kwa sasa

25 Oktoba 2024

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amelipinga ombi la Ukraine kujiunga kwa dharura na jumuiya ya kujihami, NATO lililowasilishwa na Rais Volodymyr Zelenskyy.

https://p.dw.com/p/4mCtb
Kansela wa ujerumani Olaf Scholz
Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz asema Ukraine haiwezi kujiunga sasa na jumuiya ya kujihami, NATO kwa kuwa iko vitaniPicha: Ebrahim Noroozi/AP/picture alliance

Kansela Scholz amesisitiza alipozungumza ba shirika la utangazaji la Ujerumani la ZDF kwamba, ni muhimu kutambua kwamba hilo haliwezekani kwa kuwa nchi iko vitani.

Wiki iliyopita, Zelenskyy aliwataka viongozi wa Ulaya kukubali ombi la kuipa uanachama wa NATO kama sehemu ya "Mpango wake wa Ushindi" wa kumaliza vita ifikapo 2025.

Katika hatua nyingine, Idara ya kijasusi ya kijeshi ya Ukraine jana ilidai kuwa wanajeshi wa Korea Kaskazini tayari wamepelekwa kwenye eneo la Kursk, kuliko na mpaka wa Urusi ambalo Ukraine ambako Ukraine ilifanya mashambulizi hivi karibuni.

Idara za kijasusi zinadai kuwa takriban wanajeshi 12,000, wakiwemo maafisa 500 na majenerali watatu, sasa wanajiandaa kuingia kwenye vita hivyo.

Katika taarifa, Kyiv alisema, "Moscow imemteua Naibu Waziri wa Ulinzi wa Urusi Yunus-Bek Yevkurov kusimamia mafunzo ya wanajeshi hao wa Korea Kaskazini."

Rais wa Urusi Vladmir Putin, akizungumza katika mkutano wa kilele wa BRICS aliouandaa katika mji wa Kazan, hakukanusha kuwa wanajeshi wa Korea Kaskazini wako nchini Urusi kwa ajili ya kupelekwa Ukraine, akisema tu kwamba "Tunashirikiana na marafiki zetu wa Korea Kaskazini.