Scholz atoa wito kwa wakulima kabla ya maandamano
14 Januari 2024Matangazo
Maandamano hayo mapya ni kwa ajili ya kupinga mipango ya serikali inayobatilisha punguzo la kodi ya kilimo.
Scholz katika ujumbe wake amesema ingawa maandamano ambayo ni halali lakini yakigeuka na kuwa ghadhabu au yakipuuza michakato na taasisi za kidemokrasia, basi pande zote zitapoteza.
Maandamano hayo ya wakulima yamesababisha msongamano kutokana na matrekta ya wakulima kuzuia barabara ambapo magari makubwa yanayosafirisha bidhaa katika jiji la Berlin na maeneo mengi ya nchi, yamekwama kwenye misongamano.
Maelfu ya wakulima wanatarajiwa kuhudhuria kilele cha maandamano ya wakulima yatakayofanyika katika mji wa Berlin siku ya Jumatatu. Tukio hilo pia linaungwa mkono na sekta ya usafiri, madereva wa malori na wasambazaji wa mizigo.