Scholz azuru Korea Kusini, baada ya mkutano wa G7 Japan
22 Mei 2023Matangazo
Hayo ni wakati Ujerumani na Korea Kusini zikiajiandaa kusaini makubaliano ya kuimarisha ushirikiano wa ulinzi. Rais wa Korea Kusini Yoon Suk-yeol alitangaza jana muafaka huo wakati wa ziara ya Scholz mjini Seoul.
Alisema unalenga kuzilinda siri za kijeshi na kusaidia kuendesha kwa urahisi ugavi wa sekta ya ulinzi. Scholz alisema majaribio ya makombora ya Korea Kaskazini ni ishara ya "hali bado kuwa hatari" kwenye rasi ya Korea.
Soma pia: Kansela wa Ujerumani Scholz kuhudhuria mkutano wa G7 Ijumaa
Scholz alizuru Korea Kusini jana, baada ya kuhudhuria mkutao wa kilele wa G7 mjini Hiroshima, Japan. Ndiye Kansela wa kwanza wa Ujerumani kuzuru mji mkuu wa Korea Kusini kwa mkutano wa pande mbili katika kipindi cha miaka 30.