Senegal kukutana na Nigeria, Sudan kwenye CHAN
16 Januari 2025Matangazo
Michuano hiyo itaandaliwa kwa pamoja na Kenya, Tanzania na Uganda Agosti mwaka huu. Mashindano hayo yanayofanywa kila baada ya miaka miwili, yamesogezwa miezi sita mbele ili kuzipa nchi hizo tatu muda zaidi wa kukamilisha kujenga na kuboresha viwanja vitakavyotumika.
Kundi D pia litajumuisha Kongo Brazzaville. Harambee Stars wa Kenya wamepangwa katika Kundi A pamoja na mabingwa mara mbili na ambao walifika nusu fainali ya Kombe la Dunia 2022 Morocco, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Angola na Zambia.
Kundi B lina Tanzania, Madagascar, Mauritania, Burkina Faso na Jamhuri ya Afrika ya Kati. Wenyeji wenza Uganda watacheza katika Kundi C pamoja na Niger, Guinea na timu nyingine mbili ambazo bado hazijajulikana.