Senegal yaweka ajenda kabambe ya maendeleo
15 Oktoba 2024Rais wa Senegal Bassirou Diomaye Faye, ameutaja mfumo huo mpya wa sera ya umma kama "maono kwa Senegal ambayo inatamani sio tu kushiriki katika ulimwengu wa kesho, lakini kuchukua jukumu kubwa ndani yake".
Faye ameongeza kuwa agenda ya mabadiliko ya kitaifa ya Senegal 2050, itafanya kazi kuifanya nchi hiyo kuwa mshirika mkuu wa kikanda na mfano wa maendeleo kwa Afrika.
Sonko asema mpango mpya wa serikali utaiondoa Senegal katika utegemezi wa mataifa ya nje
Waziri mkuu wa Senegal Ousmane Sonko, amesema mkakati huo ulilenga kuvunja kile alichokiita "mtindo wa kujirudia wa utegemezi na maendeleo duni.
Mpango huo wa miaka 25 unalenga kuliondoa taifa hilo la Afrika Magharibi kutoka katika utegemezi wa mataifa ya kigeni na madeni na kutumia raslimali za ndani.