Seneti ya Kenya kupiga kura kumuondoa naibu rais mamlakani
17 Oktoba 2024Matangazo
Gachagua anakabiliwa na madai ya ubadhirifu wa fedha za umma, kuchochea ukabila na kuihujumu serikali, madai ambayo anayakana. Iwapo theluthi mbili ya maseneta wataunga mkono kuondolewa ofisini kwa Gachagua katika kura ya jioni ya Alhamisi, Gachagua atakuwa naibu wa rais wa kwanza nchini Kenya kuondolewa madarakani kwa njia hiyo iliyoanzishwa kupitia katiba mpya ya nchi hiyo ya mwaka 2010.
Siku ya leo itajumuisha ushahidi utakaotolewa na Gachagua mwenyewe ambaye atajibu madai kadhaa yaliyowasilishwa na mbunge Mwengi Mutuse.
Mahakama za Kenya zimekataa kusimamisha vikao hivyo vya Baraza la Seneti kama alivyotaka Gachagua, ila zimesema kwamba huenda zikauangazia upya mchakato huo iwapo umefuata sheria mara utakapokamilika.