1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Seoul.Korea ya Kusini yaanza kutekeleza vikwazo dhidi ya Korea ya Kaskazini.

26 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CCz1

Licha ya onyo kali lililotolewa, Korea ya Kusini imechukua hatua ya kwanza katika kutekeleza vikwazo vya Umoja wa Mataifa iliyoviwekea Korea ya Kaskazini kufuatia jaribio la kinyuklia.

Seoul imesema itawazuia maafisa wa Korea ya Kaskazini wasiingie nchini mwake kuambatana na vikwazo vya usafiri vya Umoja wa Mataifa.

Mapema Marekani ililipuuza onyo la Korea ya Kaskazini lililodai kuwa lina lengo la kuigawa jumuiya ya kimataifa.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa sauti moja lilipiga kura ya kuiwekea vikwazo vya fedha na silaha dhidi ya Korea ya Kaskazini baada ya kufanya jaribio lake la kwanza la kinyuklia mapema mwezi huu.