Sera za Trump za uzalendo hazibadiliki
1 Februari 2018Mhariri wa gazeti la Saarbrücker Zeitung anaandika kwamba kuna ujumbe wa aina mbili , ambao Donald Trump aliutuma: Marekani imo katika njia sahihi, na Marekani sio tu imara, lakini pia iko tayari kutumia nguvu zake. Mhariri anaendelea:
Rais wa marekani anapaswa kutambua kwamba hali hii inatokana tu na mabadiliko ya uongozi katika Ikulu ya Marekani ya White House. Ni mtazamo wa mtu anayejipenda binafsi, ambaye kila mara hujiweka mbele kwa kila kitu. Kama ilivyokuwa kwa mmoja kati ya wangulizi wake , hususan George W. Bush ambaye anamkaribia , anaelekea katika mwendo wa kuyumba yumba. Ni matarajio yetu, kwamba hataifuata kwa muda mrefu njia ya nchi aitakayo.
''Mtu aliyejifunika joho la hamasa za uzalendo , ameelezea kwa hali ya kufadhaisha hali ya taifa'' Mhariri wa gazeti la Berliner Zeitung anaandika. Nusu karne baada ya kuuwawa kwa Martin Luther King Marekani imegawika kuliko wakati mwingine wowote. Hili si kosa pekee la Donald Trump. Mhariri anaendelea:
Siasa zake za mikakati ya matumizi ya kimabavu na uongo zinaonekana kila siku. Hotuba yake ya dakika 80 siku ya Jumapili katika baraza la Congress haziwezi kabisa kubadilika.
Gazeti la Neue Osnabrücker Zeitung linazungumzia kuhusu muungano mkuu , katika majadiliano ya kuunda serikali ya mseto nchini Ujerumani kati ya vyama ndugu vya CDU/CSU pamoja na kile cha kisoshalist cha SPD. Mhariri anaandika kwamba kutokana na ongezeko la wazee nchini Ujerumani wafanyakazi wengi zaidi wa kuwahudumia wazee ni lazima waongezeke. Hayo ni kwa mujibu wa majadiliano yanayoendelea ya kuunda serikali ya mseto. Mhariri anaendelea:
Haya ni maendeleo yaliyotakiwa kufanyiwa kazi tangu muongo mmoja uliopita. Lakini sasa yanapaswa kutekelezwa. Pamoja na hayo mabadiliko haya yanahitaji muda . watapatikana wapi mara moja wafanyakazi 8,000, ambao kupitia mpango huo wa haraka wataweza kuajiriwa. Kwa hiyo itachukua muda , hadi pale wafanyakazi wapya watakapopata mafunzo. Kwa malipo bora itawezekana kazi hiyo ya kuwahudumia wazee ikawavutia watu tena. Kile ambacho vyama vinavyotaka kuunda muungano vimekinyamazia , ni zitatoka wapi fedha za kugharamia malipo ya juu ya wafanyakazi katika sekta hiyo ya kuwapa huduma wazee.
Kuhusu Ziara ya waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani nchini Israel, gazeti la Badische Zeitung la mjini Freiburg linaandika.
Kitojo:
Mwaka uliopita baada ya kutokea hali ya kutokuelewana mazungumzo kati ya waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani na waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu karibu yavunjike kabisa. Kwa kutumia busara , Gabriel hakukata tamaa , badala yake alilizunguka suala la kuwapo mataifa mawili na kuzungumzia suala la ushawishi wa Iran katika eneo hilo. Anapozungumza Netanyahu , Israel haisaidiki.
Mwandishi: Sekione Kitojo / Inlandspresse
Mhariri: Gakuba, Daniel