Serengeti- Safari kuelekea kusikojulikana/ Artikeltext B
17 Aprili 2014Leo warithi wao wanaisimamia mbuga hiyo ya taifa. Timu ya Afrika ya Jumuiya ya Kutunza Wanyama ya Frankfurt (FZS) inatoa kipaumbele cha juu kabisa kwa mbuga ya wanyama ya Serenegeti. Na leo hii, Serengeti ni miongoni mwa mbuga za wanyama zenye ulinzi bora zaidi duniani. Lakini maisha ya wanyamapori huko yanazihisi athari za ulimwengu wa kisasa. Hiyo inatoa changamoto kwa watunzaji wa wanyama. Kwa mfano, jumuiya ya FZS iliweza kuzuwia ujenzi wa barabara kuu kupitia katika mbuga hiyo. Barabara hiyo ingeweza kuvuruga uhamaji wa wanyama na kuharibu mfumo wa ikolojia wa Seregenti katika muundo wake wa sasa.
Mbuga hii hufadhiliwa kwa kiasi kikubwa kupitia malipo yanayotozwa kwa wageni. Kiasi kingine cha euro milioni moja kutoka mjini Frankfurt kila mwaka, hutumiwa katika ulinzi wa Serengeti. FZS inatumia fedha hizo kuisaidia Mamlaka ya Mbuga za Wanyamapori ya Tanzania (TANAPA) katika programu zake za mafunzo na uendeshaji, au kuipatia vifa vya ufundi kama vile magari yanayotumiwa na wasimamizi wa mbuga. Bila ushirikiano huu na kujitolea bila kuchoka kwa wahifadhi, wanyama wa Serengeti wangekabiliwa tena na maangamizi.
Mwandishi: Inga Sieg
Tafsiri: Iddi Ssessanga
Kamera na Picha: Axel Warnstedt
Sauti: Moritz Polomski
Uhariri: Klaudia Begic