1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Serikali kujadili tafiti za mabadiliko ya tabianchi

13 Machi 2023

Wanadiplomasia kutoka takriban nchi 200 pamoja na wanasayansi wa mabadiliko ya tabia nchi leo wanaanza mkutano wa wiki moja nchini Uswisi.

https://p.dw.com/p/4OcBg
Eisbär Eisbären Klimawandel Eisscholle Symbolbild
Picha: picture alliance/dpa

Mkutano huo unalenga kujadili utafiti wa kisayansi wa takriban muongo mmoja uliopita, na kuandaa chapisho moja la kurasa 20, kutoa tahadhari kuhusu hatari iliyopo ya ongezeko la joto duniani na hatua zinazopaswa kuchukuliwa.

Ripoti hiyo inayotarajiwa kutolewa Machi 20, ya jopo la Umoja wa Mataifa linawaloleta pamoja wawakilishi kutoka serikali mbalimbali kuhusu mabadiliko ya tabia nchi (IPCC), itaainisha mabadiliko ambayo yametokea, na yanayotarajiwa kutokea ulimwenguni siku zijazo, kwenye mfumo wa tabia nchi kama vile mawimbi ya joto, mafuriko na ongezeko la kina cha maji baharini.

Tangu mwisho wa karne ya 19, kwa wastan, joto la dunia limeongezeka kwa zaidi ya nyuzi 1.1 kwenye vipimo vya Celsius, kiasi hicho kinatosha kusababisha majanga yanayofungamana na hali ya hewa katika kila bara.