1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaVenezuela

Serikali, upinzani Venezuela wakubaliana uchaguzi mwakani

Josephat Charo
18 Oktoba 2023

Serikali ya Venezuela na upinzani wamekubaliana katika duru mpya ya mazungumzo kwamba uchaguzi wa rais utafanyika nusu ya pili ya mwaka ujao na waangalizi wa kimataifa watakuwepo.

https://p.dw.com/p/4Xfh3
Venezuela I Nicolas Maduro
Picha: Matias Delacroix/AP/picture alliance

Makubaliano kuhusu uchaguzi huo yamesainiwa huko Barbados kufuatia mazungumzo yaliyoongozwa na Norway yaliyoanza siku ya Jumanne (Oktoba 17) pamoja na ahadi ya kuzialika timu za kiufundi za waangalizi wa uchaguzi za kimataifa.

Soma zaidi: Lula na Maduro wazindua "zama mpya" za uhusiano kati yao

Miongoni mwa waangalizi watakaolikwa ni wa Umoja wa Ulaya, Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika na Jumuiya ya Tume za Uchaguzi za Mabara ya Amerika.

Kwa mujibu wa mkataba uliosainiwa tarehe halisi ya uchaguzi itaamuliwa na tume ya kitaifa ya uchaguzi ya Venezuela.