1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaEthiopia

Ethiopia: Hali ya hatari yatangazwa kwenye jimbo la Amhara

4 Agosti 2023

Serikali ya shirikisho ya Ethiopia lmetangaza Hali ya hatari wakati ambapo mapigano makali yanaongezeka kati ya jeshi la taifa na Wanamgambo katika eneo la kaskazini la Amhara.

https://p.dw.com/p/4UnGZ
Abiy Ahmed Ali | äthiopischer Premierminister
Picha: Massimo Percossi/Ansa/ZUMA Press/IMAGO

Ofisi ya waziri mkuu Abiy Ahmed imetangaza uamuzi huo baada ya kiongozi wa kanda ya kaskazini kusema kwamba vikosi vya jimbo hilo haviwezi tena kudhibiti vurugu zinazoendelea.

Wiki hii, wakaazi wameripoti mapigano katika eneo lote la Amhara huku wanamgambo wakishambulia vitengo vya jeshi na waandamanaji waliofunga barabara. Safari za ndege kwenye miji miwili maarufu ya kitalii, Lalibela na Gondar, zimesimamishwa. Huduma za intaneti pia zimeathirika.

Wakimbizi wa ndani katika jimbo la Amhara la kaskazini mwa Ethiopia.
Wakimbizi wa ndani katika jimbo la Amhara la kaskazini mwa Ethiopia.Picha: Alemnew Mekonen/DW

Waziri Mkuu wa Ethiopia ameserma ni muhimu kutangaza hali ya hatari kutokana na kwamba ni vigumu kudhibiti vuguvugu lisilokubalika chini ya sheria ya sasa. Hata hivyo taarifa hiyo kutoka ofisi ya Waziri Mkuu haikuweka wazi ikiwa hali hiyo ya hatari inahusu nchi nzima au kwa jimbo la Amhara tu lilioko kaskazini mwa mji mkuu, Addis Ababa.

Abiy Ahmed amesema usalama wa taifa na wa umma unaendelea kutishiwa siku baada ya siku ambapo amebainisha kuwa hali hiyo inaharibu uchumi na wakati huo huo ameyalaumu makundi yanayofuata itikadi kali.

Jimbo la Amhara la pili kwa kuwa na watu wengi nchini Ethiopia linakabiliwa na ukosefu wa utulivu tangu mwezi Aprili, wakati serikali kuu ilipotangaza kuwa inasambaratisha vikosi vya kikanda baada ya kumalizika mapigano yaliyodumu kwa miaka miwili katika mkoa jirani wa Tigray. Vikosi vya eneo la Amhara na wanamgambo wa eneo hilo waliliunga mkono jeshi la taifa katika vita vyake vya miaka miwili dhidi ya waasi kutoka eneo jirani la Tigray.

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed
Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy AhmedPicha: Office of the Prime Minister Ethiopia/UPI Photo/Newscom/picture alliance

Mamlaka ya Ethiopia mnamo mwaka jana pia ilijaribu kulisambaratisha kundi lisilo rasmi la wanamgambo wa Amhara lililojulikana kama Fano ambapo wazalendo katika eneo hilo la Amhara walihisi kuwa hatua hiyo ingelidhoofisha jimbo lao.

Mgogoro huo ulitatuliwa kwa makubaliano ya amani mnamo Novemba 2022 lakini vikosi maalum vya Amhara na wapiganaji wa kundi la wanamgambo wa Fano wanaendelea kudhibiti eneo la kaskazini mwa Tigray, lenye rutuba na linalozozaniwa na Tigray na Amhara.

Ni machafuko ya hivi karibuni kuikumba Ethiopia tangu Waziri Mkuu Abiy Ahmed aingie madarakani mnamo mwaka 2018 na kuahidi kulifungua moja kati ya mataifa ya barani Afrika yaliyo na vizuizi kwenye mifumo yake ya kisiasa na kiuchumi.

Vanyzo:AP/AFP