1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Serikali ya Ethiopia yatishia kufanya operesheni tena Tigray

15 Julai 2021

Viongozi wa Ethiopia wamesema wako tayari kufanya operesheni mpya ya kijeshi dhidi ya maadui, baada ya waasi kusonga mbele na kuingia ndani zaidi katika jimbo Tigray.

https://p.dw.com/p/3wWIm
Äthiopien I Konfliktregion Tigray
Picha: Ethiopian News Agency/AP/picture alliance

Hali hiyo inatishia hatua iliyotangazwa na serikali ya kusitisha mapigano katika eneo hilo linalokabiliwa na mgogoro.

Vikosi vya waasi wa Tigray wiki hii vilidai kupata mafanikio zaidi baada ya kudhibiti sehemu kubwa ya mkoa huo wa kaskazini wiki mbili zilizopita ambapo vikosi vya Tigray viliudhibiti tena mji mkuu wa Tigray, Mekele baada ya eneo hilo kutumbukia kwenye vita kwa muda wa miezi minane.

Waziri Mkuu Abiy Ahmed, amesema serikali yake ilitangaza kusitisha mapigano mnamo Juni 28 kwa sababu ilichagua amani kwa matumaini kwamba mapigano yatasimama kabisa hali itakayowawezesha wakulima kupanda mazao ya chakula na wakati huo huo kuwezesha misaada kupelekwa katika mkoa huo uliokumbwa na vurugu.