Serikali ya Togo yakiri yaliomo katika ripoti ya haki za binaadamu.
27 Septemba 2005Matangazo
Lome:
Serikali ya Togo imeungama kwamba majeshi yake ya usalama yalitumia nguvu za kupita mpaka kuvunja ghasia za kisiasa mapema mwaka huu. Kukiri huko kwa serikali ya nchi hiyo, kunafuatia ripoti ya umoja wa mataifa kuhusu haki za binaadamu, ambayo imeilaumu serikali kwa sehemu kubwa ya machafuko hayo ambapo karibu watu 500 waliuwawa na maelfu kujeruhiwa , baada ya upinzani kupinga matokeo ya uchaguzi wa Rais mwezi Aprili, ukidai uliandamwa na wizi mkubwa wa kura. Serikali imesema itaichunguza ripoti hiyo katika hali ya uwazi.