Serikali za Kenya na Tanzania kufaidika na ujenzi wa barabara.
22 Aprili 2013Mkopo huo wa Dola Milioni 232.5 umethibitishwa na Benki ya maendeleo ya Afrika AFDB,katika kufaninkisha mradi wa barabara hiyo ili kurahisisha huduma za usafiri na muingiliano wa kimasoko wa nchi za umoja wa Afrika Mashiriki.
Mkurugenzi wa Benki ya maendeleo ya Afrika AFDB kanda ya Afrika ya Mashariki, Gabriel Negatu,amethibitisha mkopo huo na kusema kuwa ujenzi wa barabara hizo tayari ulikuwa katika mkakati wa kanda ya Muingiliano wa Afrika Maashariki RISP wa mwaka 2011-2015.
''Jumuiya Afrika Mashariki inahitaji kuimarisha miundombinu ya usafiri katika kanda hii,ili kuhimiza maendeleo ya kiuchumi,mpango wa maendeleo ya jamii,kuvutia utalii na muingiliano wa kijamii katika kanda hiyo wakati huo huo kurahisisha biashara katika mipaka hiyo na biashara za kimataiafa''Amesema Gabriel Negatu.
Katika mradi huo,Serikali ya Kenya itapokea mkopo wa Dola za Marekani milioni 113.3 katika jumla ya mkopo waote wa milioni 232.5 unaotolewa na Benki hiyo,wakati Tanzania itapokea kiasi cha Dola milioni 120,na Banki hiyo itachangia asilimia 89 ya gharama za mradi wote.
Ujenzi wa barabara
Ujenzi huo ambao unadhaminiwa na serikali ya Kenya na Tanzania unatarajiwa kukamilika Desemba mwaka 2018 ambapo serikali zote mbili zimechangia kiasi cha Dola milioni 15.6 na Dola milioni 12.3,huku mfuko wa biashara wa Afrika ukichangia kiasi cha Dola asilimia 0.17 milinio,kwa ajili ya kuandaa miundombinu ya biashara katika eneo mpaka wa Namanga,ikiwa jumla ya ghrama zote za mradi huo Dola milioni 262.2.
Barabara ya Arusha-Holili na Taveta-Voi ni chemba muhimu ya usafiri katika ukanda wa Afrika Mashariki,ambayo inaunganisha Chemba ya Kaskazini katika eno la Voi kwenda Chemba ya Kati kupitia mpaka muhimu eneo la Holili-Taveta kutokezea Arusha,Babati hadi Dodoma na Singida.
Mradi huo utawahusisha wafanyakazi wa maeneo husika katika ujenzi wa baeabara inayopita Arusha ya kilomita 42.4 pamoja na uekaji huduma za barabarani pembeni ya barabara zote mbili.
Mabali na hilo mradi huo utakarabati kipande cha barabara ya Mtetwa-Taveta nchini Kenya ambacho kina ukubwa wa kilomita 89 pamoja na kipande cha barabara ya kupitaia Taveta cha kilomita12 na hudumna zote za barabarani katika eno la Bura,na Maktau katika barabara ya Mwatate-Taveta nchini Kenya.
Barabara ya Arusha-Holila na Taveta-Voi ni moja ya Chemba muhimu ya usafiri katika Kanda ya Afrika Maashariki ikiwa na lengo la kuimarisha na kurahisisha shuguli za kibaishara na kuongeza ushindani wa kimasoko wa kanda hiyo katika masoko ya kimataiafa na kuweka muingiliano mzuri katika nchi hizo.
Endapo mradi huo wa barabara utakamilika,utaunganisha bandari ya Mombasa upande wa Kaskazini nchini Kenya,na Kaskazini ya Mashariki ya Tanzania pamoja na nchi zisizokuwa na bandari za Burundi,Rwanda,DRC na Uganda na kuandaa njia mbadala ya baharini.
Benki ya Maendeleo ya Afrika mashariki,ni taasisi ya maendeleo ambayo imeanzishwa kwa lengo la kuchangia katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa nchi za Afrika,ambapo Benki hiyo inajumuisha vitengo vikuu vitatu,kitengo cha maendeleo cha Afrika AFDB, mfuko wa maendeleo wa Afrika ADF na mfuko wa udhamini wa Nigeria NTF.
Mwandishi:Hashim Gulana
Mhariri: Mohammed Khelef