1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Shambulio la Iran kwa ngome za marekani ni mwisho wa kisasi?

Angela Mdungu
9 Januari 2020

Miongoni mwa yaliyoandikwa na wahariri wa magazeti hapa Ujerumani ni pamoja na mzozo wa Iran na Marekani, pamoja na uchambuzi wa hatua ya uturuki kupeleka vikosi Libya.

https://p.dw.com/p/3VvoL
Ayatollah Ali Khamenei Teheran Iran
Picha: picture-alliance/abaca/SalamPix

Gazeti la Stuttgater Nachrichten limeandika kuwa hakuna anayeweza kusema iwapo makombora ya roketi yaliyozishambulia ngome mbili za Marekani nchini Iraq ndio mwisho wa mpango wa kisasi wa Iran baada ya kuuawa kwa Jenerali Qasem Soleimani. Shambulio dhidi ya Marekani kipindi hiki lilikuwa tofauti kwani halikufanywa na makundi ya wabeba silaha wa msituni. Lilifanywa moja kwa moja na serikali ya Iran kama alivyotaka kiongozi wa juu  wa  taifa hilo Ayatoullah Ali Khamenei

Kwanini majeshi ya Uturuki yaende Libya sasa?

Baada ya Uturuki kutangaza kupeleka vikosi nchini Libya siku chache zilizopita mhariri wa   Hannovischer Allgemeine Zeitung anauliza, ni kwanini Rais Erdogan anatuma jeshi lake nchi ya mbali namna hii sasa? Jibu linaloumiza si tu kwa Umoja wa Ulaya bali pia kwa Marekani ni kwamba, ni kwa sababu anao uwezo wa kufanya hivyo. Nchi za Magharibi hazina umoja na zinakosa mkakati wa pamoja, na hili linatoa nafasi zaidi kwa wenye majeshi yanayotaka kufanya majaribio ya uwezo wao.

Muungano CDU na wanachama wa SED unawezekana?

Gazeti la Die welt linauliza iwapo viongozi wa chama cha CDU kitaweza kukaa meza moja wanachama wa SED ama ilikuwa ni ndoto waliyoota katika jengo la makao makuu ya CDU liitwalo Konrad Adenauer? Kuna kauli ya wazi kuwa hakuna muungano wa CDU na die Linke wala AFD. Hakuna mbadala! Lakini neno hakuna mbadala halisaidii wala halitekelezeki kwa upande wa Ujerumani Magharibi kwa muda mrefu sasa. 

Nalo gazeti la  Badische Neueste Nachrichten limeandika kuhusu mkutano wa chama cha CSU huko Seeon, Munich. Linaandika hakika jambo muhimu katika mtazamo wa kiongozi wa chama cha CSU baada ya ushiriki wake katika mkutano wa chama cha CDU mnamo mwezi Novemba mwaka jana kiongozi huyo, amejidhihirisha kama mtu anayetoa msukumo, na mwelekeo sahihi wa umoja wa vyama hivyo. Kwa Annegret Kramp-Karrenbauer hali haimsumbui. Baada ya mkutano wa Leipzig yeye ni mwenyekiti wa CDU aliye katika muda wa majaribio. CSU yenye nguvu ikiwa upande wake itaongeza ufanisi katika nafasi yake.