1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Shambulio la umwagaji damu Istanbul

15 Novemba 2003
https://p.dw.com/p/CEDF

ISTANBUL: Nchini Uturuki umetokea mripuko mkubwa karibu ya hekalu kubwa kabisa ya Kiyahudi mjini Istanbul. Kufuatana na ripoti za mwanzo kutoka vyombo vya habari vya Kituruki, wameuawa watu 11 na kujeruhiwa 30 wengine. Inadhaniwa kitazidi kuongezeka kiwango hicho cha vifo. Mripuko huo ulikuwa na nguvu zilizoteketeza maduka na magari kadha kwenye barabara inayopitia kituo cha mripuko huo. Kingali bado hakijulikani chanzo cha mripuko huo. Wakati huo huo walijeruhiwa watu kadha wengine ulipotokea mripuko wa pili katika kituo kingine mjini Istanbul. Pia hakijulikani chanzo cha mripuko huo. Hekalu kubwa ya Neva Shalom iliyopo katikati ya Istanbul iliwahi kushambuliwa kwa bomu mwaka 1986. Wakati ule waliuawa watu 24.