1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Shambulio mjini Istanbul ni ujumbe kutoka IS

Admin.WagnerD13 Januari 2016

Wahariri wa magazeti ya Ujerumani wamejishughulisha sana na shambulio la kigaidi mjini Istanbul, na pia kuhusu sheria ya kuwarejesha makwao watu wanaoomba hifadhi Ujerumani watakaopatikana na hatia ya kufanya uhalifu.

https://p.dw.com/p/1HcMI
Türkei Touristen verlassen Istanbul nach dem Anschlag
Watalii wengi wakiondoka kutoka Uturuki baada ya shambulio la kigaidiPicha: picture-alliance/epa/C. Turkel

Tukianza na gazeti la Stuttgarter Nachrichten, likizungumzia shambulio la kigaidi mjini Instanbul Uturuki mhariri anaandika:

"Ni mara chache Waislamu wenye itikadi kali wanawakaribia Wajerumani. Lakini sio tu, kwamba mshambuliaji wa kujitoa muhanga ameweza kuwauwa Wajerumani wengi na kuwajeruhi wengine. Pekee uchaguzi wa eneo lenyewe ambalo ni sehemu inayovutia watalii wengi barani Ulaya kufanya uhalifu huo hali hiyo inaathari za nguvu za kishetani."

Wajerumani wengi wanalifahamu eneo hilo kwa kulitembelea ama kuliona tu katika vyombo vya habari au televisheni.

Kwa shambulio hilo magaidi wanatuma ujumbe , kwamba inawezekana kuwafikia "kila mmoja wenu". Kila mahali. Lakini sio hivyo. Hawana uwezo huo.

Mhariri wa gazeti la Neue Osnabrücker nae anazungumzia kuhusu shambulio hilo la kigaidi mjini Istanbul.

"Shambulio dhidi ya watalii mjini Istanbul linatisha. mtu anajiuliza ; kitu gani kinakuja baada ya hapa ? Kuna athari gani ya mashambulizi ya kigaidi mjini Paris na hofu ya kutokea shambulio mjini Brussels. Mtu yeyote anaweza kuguswa na vitendo hivyo, wakati akiwa katika shughuli zake.

Ni ushahidi wa kitisho kikubwa cha wanamgambo wa kundi la Dola la Kiislamu. Na hali hiyo haina uhusiano wowote na Uislamu? Wengi wa Waislamu wanajitenga na hali hiyo, na mtu anaweza kuelewa. Lakini inawezekanaje kufikia mwisho wa mauaji haya ya kujitoa muhanga , wakati kuna hisia hizi za kwenda peponi , ambapo mtu anayewauwa wenzake kwa bomu, anafikiri kuwa atazawadiwa wanawake 72 peponi na sio kwenda motoni."

Nae mhariri wa gazeti la Nordbayerischer Kurier akizungumzia kuhusu shambulio hilo la mjini Istanbul , anasema;

"Kabla hata marubani wa ndege za Tornado za Ujerumani kwenda katika kituo cha usaidizi cha NATO nchini Uturuki katika mji wa Incirlik , kufanya uchunguzi katika eneo linalodhibitiwa na kundi la kigaidi la IS nchini Syria, kijana kutoka Syria alijiripua katikati ya kundi la watalii kutoka Ujerumani mjini Istanbul." Mhariri anaandika:

"Watalii wanane Wajerumani jana asubuhi waliuwawa. Wanamgambo wa Dola la Kiislamu sasa wametangaza rasmi vita dhidi ya Ujerumani."

Mshambuliaji wa kujitoa muhanga ameichoma mkuki Uturuki katikati ya moyo wake na kuwauwa watu kadhaa, ambao walikuwa tu katika mapumziko anaandika mhariri wa gazeti la Mannheimer Morgen. Mhariri anaendelea kuandika:

"Inaonekana kama kitu cha kawaida , kwamba hapo zamani kulikuwa pia na matukio ya mashambulizi ya kigaidi nchini Uturuki na watu wengi tu waliuwawa. Lakini mara hii hakuna Mturuki aliyeuwawa, badala yake ni wageni. Ghafla dunia yote inaikodolea macho nchi hiyo.

Jana baadhi ya watalii walifunga masanduku yao na kurejea nyumbani. Wengi hawataweza kurejea tena nchini humo hivi karibuni , baadhi huenda hawatarejea kabisa. Na hiyo ndio athari kubwa itakayoikumba Uturuki. Utalii ni moja kati ya vyanzo muhimu vya mapato katika nchi hiyo. Baada ya Uturuki kuiangusha ndege ya kijeshi ya Urusi Novemba mwaka jana , watalii wengi kutoka Urusi hawaji tena. Kudhoofika zaidi kwa sekta hiyo ni hatari kwa Uturuki."

Mhariri wa gazeti la Die Welt anazungumzia mada nyingine , ambayo ni kuhusu kuimarishwa kwa sheria dhidi ya wageni ambao watapatikana na hatia ya uhalifu nchini Ujerumani , na kwamba watu hao warejeshwe makwao. Mhariri anaandika.

"Bila shaka uamuzi huu ni sehemu ya kuanzishwa kwa hatua bila ya mipango maalum. Lakini ni makosa kuifanya hatua hiyo kuwa haina maana na kwamba ni ya kujitafutia umaarufu tu , kwa kuwa katika nchi inayofuata sheria hatua hii si rahisi kuitekeleza na kuwarejesha wakimbizi ambao wamefanya makosa ni suala lenye utata.

Katika mjadala wa wazi hata serikali ya Ujerumani itakuwa inajiweka katika hali fulani, na inatoa ishara maalum. Kwa muda mfupi tu utamaduni mzima wa " Mnakaribishwa " umetoweka. Baada ya mkesha wa mwaka mpya mjini Cologne, serikali ya Ujerumani inatoa ujumbe mpya wenye ncha mbili kwa wananchi wake , kwamba inatambua mbinyo uliopo wa kisiasa na inachukua hatua ; na wale waliohusika katika uhalifu wataadhibiwa, hata wakiwa hapa Ujerumani."

Hayo ndio maoni ya wahariri wa hapa Ujerumani katika tahriri zao leo. Aliyewakusanyia ni Sekione Kitojo.

Mwandishi: Sekione Kitojo / Inlandspresse / dpa

Mhariri:Iddi Ssessanga