Shambulizi la Ukraine laharibu daraja la Crimea: Urusi
22 Juni 2023Shambulizi lililofanywa na Ukraine limeharibu daraja linalounganisha rasi ya Crimea na eneo la kusini mwa Ukraine ambalo kwa kiasi linadhibitiwa na Urusi.
Soma pia: Zelensky asema operesheni ya ´kujibu mapigo´ inajikokota
Gavana wa serikali iliyowekwa na Urusi katika rasi hiyo ya Crimea, Sergei Aksyonov, amesema kupitia ukurasa wa Twitter kwamba shambulizi hilo la jana usiku liliharibu daraja hilo la Chongar.
Daraja hilo linaiunganisha Crimea, iliyoanyakuliwa na Urusi kutoka Ukraine mnamo mwaka 2014, na mkoa wa Kherson.
Shambulizi hilo linafanywa wakati Ukraine ikifanya mashambulizi ya kushtukiza yenye lengo la kurejesha eneo linalokaliwa na majeshi ya Urusi na Crimea imekuwa ikilengwa mara kwa mara, na hasa kwa mashambulizi ya droni katika miezi ya hivi karibuni.