SHARON NA PALESTINA
18 Machi 2005Matangazo
JERUSELEM:
Waziri-mkuu wa Israel Ariel Sharon amelikaribisha Tangazo la kusimamisha mapigano la vikundi mbali mbali vya wsanamgambo wa kipalestina vilivyokutana nchini Misri.
Hatahivyo, waziri-mkuu Sharon amemtaka rais wa Palestina, mahmoud Abbas kuhakikisha kuwa, wanamgambo hao mwishoe wanapokonywa silaha.
Mwishoni mwa mazungumzo mjini Cairo, vikundi 13 vya wapalestina havikutaja neno "kusimamisha-mapigano" katika Tangazo lao la Cairo.Vilidai pia kuachwa huru kwa wafungwa wa kipalestina kutoka magereza ya Israel n a Israel ikome kuwaandama wapalestina katika ardhi zao walizozikalia.
Wakati Israel imelieleza Tangazo hilo kuwa ni hatua ya kwanza barabara, Marekani inadai kuwa haitoshi.