SiasaAsia
Shehbaz Sharif atarajiwa kuwa waziri mkuu wa Pakistan
14 Februari 2024Matangazo
Sharif, mwenye umri wa miaka 72, amependekezwa na chama chake cha PML-N na vyama washirika vitakavyounda serikali ya mseto kuliongoza taifa hilo lenye silaha za nyuklia.
Baada ya kuapishwa,Shehbaz Sharifatahitaji kwa mara nyingine tena kuomba mkopo kutoka kwa shirika la fedha la kimataifa IMF huku muda wa mkataba wa mkopo wa sasa ukitarajiwa kumalizika mwezi ujao.
soma pia:Vyama vya kisiasa Pakistan vyaunda serikali ya muungano
Pakistan inahitaji kuongezewa muda wa kulipa deni lake. Pakistan inaendelea kugubikwa na mzozo wa kiuchumi huku mfumuko wa bei ukisalia kuwa juu, karibu kwa asilimia 30 na wakati huo huo ukuaji wa uchumi wa nchi hiyo umepungua na kufikia karibu asilimia 2.