1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Shirika la huduma za simu Telekom lapata kiongozi mpya.

14 Novemba 2006

Shirika la huduma za simu la Ujerumani Deutsche Telekom limepata kiongozi mpya. Baada ya kujiuzulu kwa Kai-Uwe Ricke atatakiwa Rene Obermann ambaye alikuwa akiliongoza shirika la simu za mkononi la T-Mobile, kuliweka shirika hilo la huduma za simu katika hali bora kutoka katika hali ya kuporomoka. Suala la NATO kutaka kuimarisha ushiriki wa jeshi la Ujerumani Bundeswehr nchini Afghanistan ni suala jingine ambalo limezungumzwa katika udondozi wa magazeti ya Ujerumani hii leo. Mnasomewa humu studioni na Sekione Kitojo.

https://p.dw.com/p/CHUT

Gazeti la Mainz Allgemeine Zeitung linazungumzia zaidi kuhusu kiongozi huyo mpya wa Telekom. Kupatiwa kazi hiyo Obermann ametakuwa kuwa ni mtu wa kuondoa matatizo. Anatakiwa kufanya haraka kuliondoa shirika hilo katika matatizo ya kifedha. Pia kwamba wafanyakazi 40,000 kati ya wafanyakazi wake 110,000 wanahadhi ya wafanyakazi wa serikali. Wanafikiri kama wakati ambapo shirika hilo lilikuwa halina mshindani na hawa pia wanatakiwa lazima waongozwe.

Gazeti linalochapishwa mjini Bonn, General Anzeiger linaandika:

Obermann ni lazima sasa aweze kudhibiti sehemu hii ya biashara ya shirika hilo la Telekom. Ni lazima afanye haraka ili kuweza kuuzika ndani na nje ya nchi hii. Kwa hivi sasa hali haiko hivyo na inaashiria hali ya hatari kinyume chake.

Gazeti la Märkische Allgemeine linalochapishwa mjini Potsdam linawasi wasi kidogo.

Linaandika: Kama itawezekana kupandisha thamani ya hisa zake shirika hilo , bado hilo halifahamiki.

Inahitajika kuwaweka wazi kuwa wenye hiza wadogo pamoja na wenye hisa wakubwa kama serikali ya Ujerumani wanatakiwa kuwa sawa, ambapo hawatapata nafasi ya kupunguza wafanyakazi.

Iwapo Obermann ndie mtu sahihi kwa ajili ya kazi hii , ni lazima nae awe makini.

Katika gazeti la Nordbayerischen Kurier kutoka Bayreuth linaeleza hivi:

Binafsi iwapo Obermann atataka kuleta matumaini kwa pande zote, bila ya usawa na kutoa lengo kamili, anatambua wazi binafsi kuwa , upinzani utakuwa mkubwa mno. Uwezo wa shirika hili la Telekom ni lazima uongezeke kwa kiasi na ili ushindani uliokuwapo usiongezeke sana na shirika hilo la kitaifa liweze kurejea katika nafasi yake.

Tukibadilisha mada: