Shirikisho la soka Kenya kumchagua kiongozi mpya
7 Desemba 2024Wanachama wa shirikisho la soka nchini Kenya watamchagua kiongozi mpya siku ya Jumamosi, huku wasiwasi ukiongezeka kuhusu maandalizi ya nchi hiyo kuandaa Michuano ya Mataifa ya Afrika (CHAN). Wanachama wa Shirikisho la Soka la Kenya (FKF) watafanya uchaguzi wao ambao umecheleweshwa kwa muda mrefu baada ya miezi kadhaa ya mabishano na kesi.
Rais anayeondoka Nick Mwendwa alikamatwa mnamo Novemba 2021 baada ya uchunguzi wa serikali kufichua madai ya ukiukaji wa sheria za kifedha, na kamati ya muda iliundwa kusimamia shirikisho hilo.Baada ya muda mfupi shirikisho la kandanda duniani FIFA liliingilia kati na kulazimisha serikali ya Kenya kuirejesha bodi ya FKF, huku mashtaka ya ufisadi dhidi ya Mwendwa yakitupiliwa mbali baada ya serikali kukosa kutoa ushahidi wowote dhidi yake.
Soma zaidi.Kenya yaamuru kufungwa kwa mabweni ya shule 348
Mwendwa hawezi kugombea tena nafasi hiyo ya juu, akiwa tayari ametumikia mihula miwili.Lakinin uchaguzi huu unakuja katika wakati muhimu, huku Kenya ikitarajiwa kuandaa fainali za CHAN mwezi Februari. Wiki iliyopita, timu ya Shirikisho la Soka Afrika ilikagua viwanja na viwanja vya mazoezi kwa ajili ya michuano hiyo inayoandaliwa kwa pamoja kati ya Kenya, Uganda na Tanzania kuanzia Februari 1 hadi 28.