JangaChina
Watu 11 wamekufa kufuatia maporomoko ya ardhi Yunnan, China
23 Januari 2024Matangazo
Watu 11 wamekufa na wengine 47 wamenasa chini ya vifusi kufuatia maporomoko hayo ya ardhi yalitokea usiku wa kuamkia leo.
Rais wa China Xi Jinping ameagiza nguvu zote zielekezwe katika kutafuta manusura.
Vyombo vya habari vya serikali vimeripoti kuwa, uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa maporomoko hayo ya ardhi yalisababishwa na kuanguka kwa mwamba.
Zaidi ya watu 500 wamehamishwa kutoka majumbani mwao huku timu ya waokoaji 1,000 wakitumwa katika eneo la mkasa. Naibu Waziri Mkuu Zhang Guoqing anaripotiwa kuongoza timu ya waokoaji katika eneo la mkasa.
China imekumbwa na msururu wa majanga katika miezi ya hivi karibuni ikiwemo mvua kubwa za ghafla na baridi kali.