Shujaa wa filamu ya Hotel Rwanda kuachiwa huru
24 Machi 2023Rusesabagina ambaye anatumikia kifungo cha miaka 25 jela nchini Rwanda baada ya kushtakiwa kwa makosa ya kuhusika na ugaidi alihukumiwa Septemba mwaka 2021 baada ya kukutwa na hatia ya kuwa na mahusiano na mtandao unaoupinga utawala wa Rais Paul Kagame.
Kwa mujibu wa chanzo cha serikali ya Kigali, Rusesabagina kwanza atasafirishwa kwenda Doha na baadaye kupelekwa nchini Marekani. Aidha chanzo hicho kimeeleza kwamba hatua ya kuachiwa kwake imekuja baada ya shujaa huyo wa Hotel Rwanda kumuandikia barua Rais Paul Kagame kuomba ahurumiwe.
Soma pia:Majadiliano yafanyika juu ya hatma ya Paul Rusesabagina
Marekani imekuwa ikisema Rusesabagina anazuiliwa kimakosa kwa sababu ya kile ilichosema ni kukosekana haki katika undeshaji wa kesi. Rusesabagina ni raia wa Rwanda mwenye ukaazi wa kudumu wa Marekani.