Shule zafunguliwa Uganda baada ya miaka miwili
10 Januari 2022Mwalimu darasa la saba shule ya msingi ya umma ya Nakasero katikati ya mji wa Kampala. Shule hii ina wanafunzi zaidi ya elfu moja
na wameanza masomo wakizingatia kanuni zote za kudhibiti kusambaa kwa COVID-19. Miongoni mwa kanuni hizo ni kuhakikisha kuwa hakuna misongamano ya watoto sehemu yoyote na kwa hiyo wanakwenda kwa mapumziko mafupi kwa zamu.
Kwa upande wao, wazazi wanaelezea furaha yao kwamba angalau sasa watoto watakuwa katika mazingira ambayo ni salama kwao kuliko kubaki mitaani kwani wengi wamejiingiza katika vitendo viovu ikiwemo wengine kushiriki ukahaba na kupata mimba. Kero nyingine kwa wazazi ni bei ghali ya vifaa vya matumizi shuleni.
Wanaotakiwa kurejea shule
Kulingana na ratiba iliyotokewa na serikali, wanafunzi wa viwango mbalimbali watarudi shuleni kwa makundi ili kuepusha misongamano. Hii leo ni wanafunzi wa vidato vya tano na sita ndiyo wametakiwa kurudi pamoja na wale katika shule za kutwa. Mwalimu Simon Muhumuza wa shule ya sekondari amesema hivi kuhusu hali walimu wakati huu wa shule kufunguliwa.
Wazazi wengi wamelezea kuwa hawako tayari kuwarudisha watoto shuleni kutokana na changamoto kadhaa za kupata ada kwani walifutwa kazi katika kipindi hicho au mapato yao kushuka. Baadhi wameamua kuwatoa watoto kutoka shule za ada za juu ambazo nyingi ni za binafsi na wameshuhudiwa wakiwasajili katika shule za serikali.