1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sierra Leone yatangaza hali ya dharura ya Mpox

14 Januari 2025

Sierra Leone imeutangaza ugonjwa wa Mpox kuwa dharura ya afya ya umma baada ya nchi hiyo kuripoti mgonjwa wa pili wa Mpox chini ya siku nne.

https://p.dw.com/p/4p8I1
Virusi vya Mpox 2024 | Mchoro wa kifaa cha majaribio chenye matokeo ya mambukizi
Mchoro wa kifaa cha majaribio chenye matokeo yanayoonyesha mambukizi ya mpox.Picha: Dado Ruvic/REUTERS

Wizara ya afya nchini humo imesema hakuna mgonjwa yoyote kati ya hao wawili waliokutwa na Mpox aliyekaribiana hivi karibuni na wagonjwa wengine.

Inaripotiwa kwamba mgonjwa mmoja, alisafiri hivi karibuni katika mji wa Lungi ulioko wilaya ya Port Loko kaskazini kati ya Disemba 26 na Januari 6.

Wagonjwa wote wawili wanapokea matibabu katika hospitali ya mji mkuu Freetown.

Soma pia: Ugonjwa wa Mpox wazidi kuenea Burundi

Sierra Leone ilikuwa kuwa kitovu cha mlipuko wa ugonjwa wa Ebola mnamo mwaka 2014, mlipuko mbaya zaidi katika historia.

Mlipuko huo, ulioenea zaidi eneo la Afrika Magharibi, uliiathiri zaidi Sierra Leone huku vifo vya karibu watu 4,000 vikiripotiwa nchini humo kati ya vifo 11,000 vilivyorekodiwa duniani kote.

Nchi hiyo pia ilipoteza asilimia saba ya wafanyikazi wake wa kutoa huduma ya afya kutokana na mlipuko huo wa Ebola.