Ingawa hatua zimepigwa katika kupunguza utumikishwaji watoto kwa miaka mingi, miaka ya karibuni imeshuhudia mienendo ya kimataifa ikirudishwa nyuma. Maadhimisho ya mwaka huu nchini Tanzania yanafanyika mkoani Simiyu. Bruce Amani amezungumza na Mratibu wa miradi kitaifa nchini Tanzania, wa Shirika la Kazi Duniani (ILO), Glory Blasio, ambaye ametoa ufafanuzi wa kisheria wa utumukishwaji watoto.