Siku ya kimataifa ya Wanawake wa Vijijini
15 Oktoba 2018Matangazo
Dunia inaadhimisha siku ya wanawake na wasichana wa vijijini. Kauli mbiu ya siku hii inasema "Miundombinu endelevu, huduma na ulinzi wa jamii kwa usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake na wasichana wa vijijini.
Katibu mkuu wa umoja wa Mataifa Anthonio Guterres kwenye ujumbe wake amesema uwezeshaji kwa wanawake una umuhimu mkubwa katika ujenzi wa dunia yenye amani na ustawi.
Lilian Mtono amezungumza na Jael Amathi, mratibu wa programu wa shirika la Groots Kenya linaloshuguulika na uwezeshaji wa wanawake wa vijijini. Yasikilize mahojiano hayo.
Mhariri: Mohammed Khelef